Dully Sykes na Diamond kuachia Ngoma mpya ‘Chipolopolo’

d11

Mkali wa Bongo Flava, Abdul Sykes aka Prince Dully Sykes amepanga kuachia wimbo wake mpya aliyomshirikisha Diamond Platinumz, wimbo alioupa jina la ‘Chipolopolo’.

Mkali huyo ambaye wiki iliyopita video ya wimbo wake ‘Kabinti Special’ ulifungiwa kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa amekiuka maadili ya kitanzania, amesema kuwa ataachia wimbo huo hivi karibuni.
diamond1
“Hivi sasa najiandaa kuachia wimbo wangu mpya niliomshirikisha mshikaji wangu Diamond Platinumz.”Alisema  Dully.
“Ni wimbo mzuri ambao naamini mashabiki wataupenda na umetayarishwa hapa hapa studio 4.12 na mimi ndiye producer. Hivi sasa tunajipanga tu kufanya video nzuri na Adam Juma ili wimbo ukitoka uwe na video pia…na itakua hivi karibuni ila ndani ya mwezi wa tatu.”
Chipopolo inafahamika zaidi kuwa ni jina la timu ya taifa ya Zambia, jina linalomaanisha risasi za madini ya copper (copper bullets). Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Dully Sykes, wimbo huo hauiuhusu kabisa timu hiyo.
Dully Sykes na Diamond walikutana kwenye wimbo unaoitwa ‘Utamu’ wakiwa na Ommy Dimpoz na ukateka usikivu wa watu wengi. Vipi kuhusu Chipolopolo?
dully sy

JOKATE AZINDUA KIDOTI CLUB..

Image

Mrembo, Muimbaji, Muigizaji wa filamu, Mtangazaji wa TV na Mjasiriamali nchini, Jokate Mwegelo aka Kidoti jana amefanya uzinduzi wa kile alichokiita ‘Kidoti Club’.

“Ni huduma za SMS, watu wanajiunga kwenye ‘Kidoti Club’ na watakuwa watapata tips mbalimbali za urembo, mitindo na mambo ya lifestyle, inspiration… na baadae kutakuwa na zawadi za kushindaniwa,”

 

Akiongelea maboresho aliyoyafanya kwenye nywele zake za brand ya Kidoti, Jokate amesema,

Tulipotoa bidhaa za mwanzo, honestly kuna watu walisema kuna vitu ambavyo walipenda viboreshwe zaidi na sasa hivi kweli vimeboreshwa. Packaging imeboreshwa, sasa hivi tumeweka kifungo.”

“Ni bidhaa ya nyumbani, ni bidhaa inayotengenezwa na mwanamke, kwa hiyo naelewa wanawake wanahitaji nini. Ni bidhaa ambayo bei yake sio kubwa lakini quality yake ni nzuri, mtu anaweza kuvaa kwa mwezi na isimuwashe kichwani. Kwa hiyo ni kitu ambacho tumekipackage vizuri, vilevile kina muonekano mzuri, rangi tumechagua nzuri. Kwa hiyo zinashindana vizuri tu na bidhaa za nchi nyingine,” ameongeza.

Jokate amesema bidhaa zake zimeshaanza kuvuka mpaka. “Nimelenga hasa East na Central Africa, kwa sababu nimeshaanza kupata order kutoka Burundi, Kenya..yeah kwa hiyo ni East na Central Africa. Kuhusu mikoani, sasa hivi mimi nadeal kwanza na Agents, agents wangu wengi wako Kariakoo na ndio wanaopeleka mikoani. Sijaanza kupeleka moja kwa moja mikoani, hiyo ndio njia ninayoitumia kupeleka mikoani.”

 
 
 

Mganga wa Diamond aibuka tena, asema Diamond ameanza kushuka, aapa hatakufa kabla hajamuona akifulia.

Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.

Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi hata show ya milioni 7. 
Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru kwa sababu rekodi ninayo. Nimeongea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa ndio wanaonekana kuongoza.
Hata katika mambo yenu ya kumi bora za Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya.
“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana. 
Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.
“ Kwa sababu Diamond wa mwaka 2010,2011,2012 ni Diamond aliyekuwa anapiga show Mlimani City sehemu alipozaliwa Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 50,000, siku tatu kabla ya tukio tiketi zimekwisha. 
Kwa hiyo Diamond wa hivi sasa ni yule ambaye anapiga show Tabora sehemu ambayo hajawahi kuonekana, kwa kiingilio cha shilingi 5,000 na watu hawaingii na bado walioingia wanampiga mayai viza na mawe.” Ametoa mchanganuo wake.
Mtu huyo akafika mbali na kuapa, “ amini, sitakufa kabla haki hii haijatendeka, naapa…kwa heshima ya mwenyezi Mungu aliyeniumba. Anasema pigania chako ali hali hata ukifa ili mradi ulikuwa unapigania chako.”
Hata hivyo, Naseeb Abdul aka Diamond aliwahi kumkana Dr. Yahya na kueleza kuwa hamfahamu na hajawahi kumuona.
Source:Times fm.

Image