Dully Sykes na Diamond kuachia Ngoma mpya ‘Chipolopolo’

d11

Mkali wa Bongo Flava, Abdul Sykes aka Prince Dully Sykes amepanga kuachia wimbo wake mpya aliyomshirikisha Diamond Platinumz, wimbo alioupa jina la ‘Chipolopolo’.

Mkali huyo ambaye wiki iliyopita video ya wimbo wake ‘Kabinti Special’ ulifungiwa kutokana na sababu zilizoelezwa kuwa amekiuka maadili ya kitanzania, amesema kuwa ataachia wimbo huo hivi karibuni.
diamond1
“Hivi sasa najiandaa kuachia wimbo wangu mpya niliomshirikisha mshikaji wangu Diamond Platinumz.”Alisema  Dully.
“Ni wimbo mzuri ambao naamini mashabiki wataupenda na umetayarishwa hapa hapa studio 4.12 na mimi ndiye producer. Hivi sasa tunajipanga tu kufanya video nzuri na Adam Juma ili wimbo ukitoka uwe na video pia…na itakua hivi karibuni ila ndani ya mwezi wa tatu.”
Chipopolo inafahamika zaidi kuwa ni jina la timu ya taifa ya Zambia, jina linalomaanisha risasi za madini ya copper (copper bullets). Lakini kwa mujibu wa maelezo ya Dully Sykes, wimbo huo hauiuhusu kabisa timu hiyo.
Dully Sykes na Diamond walikutana kwenye wimbo unaoitwa ‘Utamu’ wakiwa na Ommy Dimpoz na ukateka usikivu wa watu wengi. Vipi kuhusu Chipolopolo?
dully sy

Leave a comment