Jay Z azidi kujidhatiti kibiashara, kuzindua Cigar yake binafsi ‘The Comador’

  1. Image
  2. Rapper mkongwe Jay Z anazidi kujidhatiti katika biashara zaidi, ambapo ripoti zinadai kuwa ameungana na kampuni ya General Cigar kutengeneza cigar yake binafsi kwa ajili ya biashara, aliyoiita ‘The Comador’.

     Tayari imeshazinduliwa tovuti maalum kwa ajili ya bidhaa hiyo inayodaiwa kuwa imetumia tumbaku zenye ubora wa hali ya juu, pia kuna akaunti za facebook na twitter kwa ajili ya ‘The Comador’.
    Tovuti ya RocNation imesema kuwa mradi huo ulikuwa katika maandalizi kwa muda wa miaka miwili. Na uzinduzi wa ‘The Comador’ unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Leave a comment